Sunday, July 4, 2010





Kwa hakika sina budi kuwashukru ndugu jamaa na marafiki leo tena na siku nyingine kama hii kpata nafasi kuwajuza angalau kidogo kuhusiana na bukumbi-maisome blogo.Ni haki na wajibu wa kila mtu kufikria na kufanya kile anachokiwaza na kumletea au kutomletea faida yoyote ile anayoifikria!

Hii ni blogo itakayo kupa fursa wewe uliye mbali karibu pengine ukiwa ni mmoja kati ya hao watakao husika katika kufanikisha habari moja hadi nyingine ikiwa na lengo la kujihusisha zaidi na kuelimisha na kufumbua japo kwa umakini kile kilicho jificha katika harakati hizi zisizo mthamini binadamu bila kujali utu na hali yake kwa ujuma.



Kwa ujumla acha nieleze hali halisi ya majina haya mawili bukumbi na maisome.Maisome ni moja ya visiwa vipatikanavyo katika wilaya ya Sengereme katika jiji la Mwanza na kina sababu ya kuitwa kisiwa sabau kuu ikiwa ni kukifikia inachukua usafiri wa maji.Meli kama Mv serengeti,Krelius na nyingine nyingi ndizo hasa hutumika kukifikia kisiwa hicho huku usafiri mwingine ukiwa ni boti ambazo huanza safari zake zikiktokea Kahunda na kukifikia kisiwa hicho.



Kutokana na masimulizi ya babu yangu hapo mwanzo kisiwa hiki hakikuwa na watu.Hakuwa na maana hawakuwepo kabisa ila walikuwa wachache ukilinganisha na sehemu nyingine nyingi za kitanzania.Upatikanaji wa watu katika kisiwa kilitokana na sababu nyingi lakini kuu zikiwa ni pamoja na UHAMISHO ULIOFANYWA NA BABA WA TAIFA HAYATI MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE,sababu nyingine ni upoteaji wa wavuvi ambao walikuwa wakikumbwa na dhoruba kali wakati wakivua samaki nakujikuta wapo sehemu hiyo.Sababu ndogondogo ni pamoja na watu kufanya maovu na kwenda kujicha mahali kama hizo kwa kuepuka mkono wa sheria ambao kwa kipndi kama hicho ulikuwa hauna mguvu za ziada kwa kuwatafuta watuhumiwa hivyo kesi pindi ziyeyukapo watu walirudi sehemu zao za asili na kusimlia sehemu hiyo ya kuvutia ambayo kwa sasa haina jina wakati ina sifa sawa na visiwa vingine kama ukerewe na vyote tuvijuavyo.



Kwa upande wa jina Bukumbi,ukiwa na miongoni mwa wafuatiliaji wa historia ya wamisainari nchini Tanzania halitkuwa jina geni kwani ni miongoni mwa sehemu za mwanzo kabisa ambazo zilitembelewa na wamisionari kwa mda usiopungua miaka 120 iliyopita na kuweka kanisa lake pale ambalo lilipewa eneo na mmoja wa viongozi wa ijadi kpindi hicho wakijulikana kama watemi.Pamoja na kufanya yote hayo pia wamisionari wamekiwezessha kiji hiki kuwa japo na mwonekano katika ramani hii ya Tanzania kwani kimejitahidi kuuanzisha taasisi mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakijipatia shughuli mbalimbali ambazo zimefanikisha katika suala zima la kipato japo kidogo lakini waut wake hunufaika nacho.Taasisis hizo ni pamoja na hospitali,shule ya sekondari ya wasichana,kituo cha kulelea wazee na walemavu,kituo cha mafunzo ya ufundi Kalwande,chuo cha makatekista namambo mengine mengi.

Nia na madhumuni ya kutumia majina haya ni katika kuboresha na kuenzi majina haya kwa nia ya kukuza amali zlizopo na kama kuna uwezekano wa mwananchi yoyote kuewekeza ni sehemu nzuri zenye kuvutia katika kutimiza yale yote yangetakiwa kuwepo sahemu hizo.

No comments: